
Kulishuhudiwa pia vurugu katika Bunge la Brazil siku ya Jumanne wakati wabunge walipokuwa wakiupigia kura muswada ambao unaweza kupunguza kifungo cha Bolsonaro mwenye umri wa miaka 70 na ambaye aligunduliwa na saratani mwezi Septemba.
Kiongozi huyo wa zamani wa Brazil kutoka chama cha siasa za mrengo wa kulia alianza kutumikia kifungo chake mwezi Novemba mwaka huu, baada ya kupatikana na hatia ya kuandaa mpango wa kumzuia Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva kuchukua madaraka baada ya uchaguzi wa mwaka 2022, kitendo kilichochukuliwa kama jaribio la mapinduzi.