Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kifo cha Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, ni pigo kubwa kwa mkoa wa Dodoma na taifa kwa ujumla, akieleza kuwa marehemu alitoa mchango mkubwa katika kuendeleza jiji hilo na shughuli za maendeleo.

Akiwa mmoja wa viongozi wa kwanza kufika nyumbani kwa marehemu Jenista Mhagama katika eneo la Itega jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule amesema Dodoma imeguswa kwa kina na msiba huu, kutokana na kazi kubwa alizozifanya marehemu wakati wa uhai wake.

@jamesbunuma
#Cloudsdigitalupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *