Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Seneti ya Marekani, Seneta Jim Risch, amekoso vikali serikali ya Tanzania kwa kufunga nchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba 2025, ili kuzuia maandamano yaliyopangwa dhidi ya vurugu za baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), Risch alisema: “Wananchi wa Tanzania waliadhimisha Siku yao ya Uhuru chini ya lockdown, pamoja na ulinzi mkali, vikwazo vya mitandao ya kijamii, na marufuku ya mikusanyiko isiyoruhusiwa ili kuzuia maandamano yanayotarajiwa. Vurugu za hivi karibuni na ufungaji wa nchi wiki hii unaonyesha kuwa Tanzania si mahali salama wala thabiti kwa uwekezaji wa Marekani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *