ARUSHA; CHAMA cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Osunyai jijini Arusha,  kimesema katika kujiimarisha kiuchumi, kipo katika mpango wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Akizungumza na DailyNerws Digital, Katibu Kata ya Osunyai, Zubeda Abdallah amesema chama hicho kina mpango wa kufanya harambee ili kujenga jengo hilo .

Amesema likikamilika jengo hilo litaongeza kipato, kwani hivi sasa kata hiyo inajivunia mradi wa upangishaji wa duka unaowezesha kupata fedha za kuendesha ofisi na ujenzi wa choo.

Amesema kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya barabara za ndani kuwa mbovu, hali inayosababisha maji kutuama haswa nyakati za mvua na wakati mwingine maji kujaa kwenye nyumba za makazi ya watu.

Amesema mvua zikinyesha  makorongo yanakuwa makubwa ndani ya kata hiyo na mitaa ikiwemo Mto Ngarenaro unaoelekea kukatika kingo zake na maji yanaelekea kwa wananchi nyakati za mvua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *