Belarus imewaachilia huru wafungwa 123 leo Jumamosi, Desemba 13, shirika la habari la serikali Belta limetangaza. Miongoni mwao ni mwanaharakati Ales Bialiatski, mpokeaji mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2022, na kiongozi wa upinzani Maria Kolesnikova, shirika la haki za binadamu Viasna limeripoti. Kuachiliwa kwa watu hao kunakuja baada ya mazungumzo kati ya Minsk na Washington.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amewasamehe “raia 123 wa nchi mbalimbali” kufuatia mazungumzo haya na Marekani, ukurasa wa Telegram Pul Pervogo, inayohusishwa na ofisi ya rais wa Belarus, imetangaza, bila kutoa majina ya watu walioachiliwa.

Maria Kolesnikova alikuwa gerezani tangu mwezi Septemba 2020 baada ya upinzani wake mkubwa dhidi ya jaribio la kumtimua katika nchi yake. Alihukumiwa kifungo cha miaka 11 jela mwaka 2021, akitumia zaidi ya miaka minne jela, ikiwa ni pamoja na mwaka mmoja na nusu katika kifungo cha upweke, bila kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki zake. Mpokeaji mwenza wa Tuzo ya Sakharov ni mmoja wa watu mashuhuri katika harakati za maandamano ya mwaka 2020 dhidi ya Rais Alexander Lukashenko.

Kuachiliwa kwake kunakuja siku moja baada ya ziara ya mjumbe wa Donald Trump nchini Belarus, ambaye alitangaza kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya potasiamu inayozalishwa na nchi hii ya Ulaya Mashariki, mshirika wa karibu wa Urusi. “Kufuatia maagizo kutoka kwa Rais Trump, sisi, Marekani, tutaondoa vikwazo dhidi ya potasiamu,” alisema John Coale, akizungumza na waandishi wa habari kutoka Minsk katika video iliyorushwa kwenye Telegram na ukurasa wa Poul Pervogo, inayohusishwa na ofisi ya rais wa Belarus.

Belarus ni mzalishaji mkuu wa potasiamu, inayotumika hasa katika utengenezaji wa mbolea. Lakini sekta hii na zingine katika uchumi wa nchi hiyo zinakabiliwa na vikwazo vikali vya Marekani na Ulaya kutokana na ukandamizaji dhidi ya upinzani nchini Belarus na uungaji mkono wa Minsk kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yaliyoanzishwa mwaka wa 2022.

Katika miezi ya hivi karibuni, Donald Trump aliihimiza Belarus kuwaachilia mamia ya wafungwa wa kisiasa nchini humo, na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, aliye madarakani kwa zaidi ya miaka 30, aliwasamehe watu kadhaa.

Kwa upande mwingine, Washington tayari iliondoa vikwazo kwa kiasi fulani dhidi ya shirika la ndege la Belarus la Belavia, ikiiruhusu kudumisha na kununua vipuri vya ndege zake, ikiwa ni pamoja na ndege za Boeing.

(Taarifa zaidi zinakujia)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *