
Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Yanga, Chico Ushindi amefariki Dunia leo Jumamosi, Desemba 13, 2025 akiwa kwao DR Congo.
Taarifa zilizothibitishwa na mmoja wa maafisa wa klabu ya Don Bosco ambayo amewahi kuitumikia akitokea TP Mazembe ni kwamba Chico amefariki baada ya kuugua kwa siku chache.
Bosi huyo amesema Chico, alikuwa sawa kiafya wiki iliyopita lakini mambo yalibadilika katikati ya wiki hii ambapo alipopelekwa hospitali Jumatano Desemba 11 hakuweza kurudi.
“Alikuwa sawa kabisa lakini ameugua siku kama tatu tu na leo tumeambiwa amefariki, viongozi walikwenda kumuona wakasema anaendelea vizuri,”amesema bosi huyo.
Chico aliitumikia Yanga kwa muda mfupi usajili wake ulitangazwa rasmi Januari 22,2022 akitokea TP Mazembe.
Wakati Chico akitua Yanga wakati huo dili hilo lilimvusha aliyekuwa kiungo wa Yanga Mukoko Tomombe akielekea Mazembe.
Hata hivyo Chico hakuweza kudumu sana ndani ya Yanga akiichezea kwa miezi sita pekeee na kurudi kwao Congo.