Katibu wa Bunge Baraka Leonard ametangaza kuwa chanzo cha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho marehemu Jenista Mhagama ni maradhi ya moyo.
Akisoma wasifu wa marehemu wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma, Katibu wa Bunge amesema kuwa marehemu alifariki dunia kufuatia changamoto za kiafya zilizotokana na maradhi ya Moyo ambayo alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Benjamin mkapa.
@jamesbunuma #Cloudsdigitalupdates