Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, ameiomba familia ya marehemu pamoja na ndugu na jamaa kuendelea kushikana na kupendana katika kipindi hiki cha majonzi, huku akisisitiza umuhimu wa kutozingatia maneno au kauli zinazoweza kuleta mgawanyiko miongoni mwao.

Akizungumza wakati wa kumuaga aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Spika Zungu amemuelezea marehemu Jenista Mhagama kuwa alikuwa mtu mnyenyekevu, mwenye kujishusha na aliyeishi kwa kuzingatia misingi ya utu na heshima. Amesema sifa hizo ni urithi muhimu ambao familia inapaswa kuendeleza ili kuhifadhi kumbukumbu njema ya marehemu.

Aidha, Spika Zungu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ushirikiano wake wa karibu na Bunge pamoja na hatua ya kutoa ndege maalum kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu pamoja na ndugu zake, hatua aliyosema imeonesha mshikamano wa kitaifa na heshima kubwa kwa mchango wa marehemu kwa taifa.

@jamesbunuma
#Cloudsdigitalupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *