Milio ya risasi mbayo chanzo chake hakijulikani imewajeruhi leo Jumamosi, Desemba 13, wanajeshi kadhaa wa Marekani na Syria ambao walikuwa sehemu ya ujumbe wa pamoja katika eneo la jangwa la Palmyra, Syria, kulingana na shirika la habari la serikali ya Syria, likinukuliwa na shirika la habari la AFP.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limebainisha kwamba “wanajeshi kadhaa wa Marekani wamejeruhiwa, pamoja na askari wawili wa vikosi vya usalama vya Syria,” walipokuwa wakifanya “ziara ya pamoja” katika eneo hilo, ambalo hapo awali lilikuwa likidhibitiwa na kundi la wanajihadi la Islamic State. Shirika hilo la habari limeongeza kwamba “mshambuliaji ameuawa.”

Hii ni mara ya kwanza tukio kama hilo kuripotiwa tangu muungano wa Kiislamu, ambao tangu wakati huo umeimarisha uhusiano wa karibu na Marekani, ulipochukua madaraka nchini Syria mwaka mmoja uliopita.

Kulingana na shirika hilo, “wanajeshi kadhaa wa Marekani walijeruhiwa, pamoja na askari wawili wa vikosi vya usalama vya Syria,” walipokuwa wakiendesha “doria ya pamoja.”

Shirika la habari la serikali ya Syria limeongeza kwamba “mshambuliaji ameuawa,” bila kutoa maelezo zaidi.

Kundi la wanajihadi la Islamic State lilidhibiti eneo la Palmyra kabla ya kushindwa nchini Syria na muungano wa kimataifa mwaka wa 2019.

Licha ya kushindwa kwake, wapiganaji wake, ambao wamerudi nyuma hadi katika jangwa kubwa la Syria, wanaendelea kufanya mashambulizi ya hapa na pale.

Shirika la habari la SANA limeripoti kwamba helikopta ziliwabeba waliojeruhiwa hadi kwenye kambi ya jeshi la anga ya Al-Tanf kusini mwa Syria, ambapo wanajeshi wa Marekani wametumwa.

Wakati wa ziara ya Rais wa mpito wa Syria Ahmad al-Sharaa huko Washington mwezi uliopita, Damascus ilijiunga na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi hilo la wanajihadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *