AFC/M23 yawataka wanajeshi wa Burundi kurejea nchini mwaoAFC/M23 yawataka wanajeshi wa Burundi kurejea nchini mwao

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bukavu, gavana wa Kivu Kusini chini ya AFC/M23, Patrick Busu Bwa Ngwi, amethibitisha kuwa mamia ya askari wa Burundi wamekamatwa katika mapigano ya hivi majuzi huko Kivu Kusini na kuwa wako salama, na kwamba watarejeshwa nchini mwao kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu, mradi tu serikali ya Burundi ifanye ombi la kurejea kwao kwa kufuata sheria za kimataifa. Patrick Busu Bwa Ngwi, anasema :

“Unajua Burundi ni nchi jirani, na hatuhitaji kupigana nao. Tumewakamata wengi na kuwaambia warudi nyumbani kufanya kazi, waache kufa hapa Kongo. Tunataka kuishi kwa amani na majirani zetu wote. Ujumbe ni kuwaita wale waliokimbia kurudi nyumbani; hakuna tatizo. Na wale vijana ambao bado wana silaha, tuleteeni silaha hizo”

Jumapili, zaidi ya Warundi 500 walioishi na kufanya kazi katika mji wa Uvira wamerudi nchini mwao baada ya kusubiri wakiwa kwenye foleni kwa muda wa siku tatu kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi. Awali, zaia hao wa Burundi waliishi na kufanya kazi mbalimbali katika mji wa Uvira.

Bado hali ni ya wasiwas Mashariki mwa Kongo

Lakini pia upande wa Burundi kunapatikana Wakongo kadhaa wanaotaka kurudi nchini mwao ila bado wamekwama kwavile mpaka wa Burundi umefungwa. kundi la AFC/M23 limedai kwamba ugumu wa kuvuka kati ya nchi hizo mbili sio kosa lake sababu mpaka uko wazi upande wa Kongo.

Kongo Goma 2025 | Waasi wa M23
Waasi wa M23 wamewataka wanajeshi wa Bundi kurejea nchini mwao, baada ya kuuteka kikamilifu mji wa UviraPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Wakati huohuo, hali ya wasiwasi inaripotiwa katika maeneo ya Makobola ambapo milio ya risasi imesikika jana kufutia vita kati ya AFC/M23 na jeshi la Kongo linaloungana na Wazalendo.

Mashuhuda wanasema wapiganaji wa AFC/M23 walifanikiwa kuteka Makobola wakielekea kijiji cha Kasekezi, wilayani Fizi. Milio ya risasi iliyofyatuliwa na askari wa Kongo wenye hasira imewapa woga wakazi wa mji wa Baraka, ukiwa mji wa tatu wa jimbo la Kivu kusini. Sammy Kalonji ni Mkuu wa wilaya ya Fizi, anaonya wakazi kutulia :

“Ninawasihi wakazi wote wa Fizi na kandokando yake wabaki kimya. Naliomba jeshi letu na Wazalendo wetu kuwatuliza miongoni mwao wanaopendelea kufyatua risasi ili kuwatia hofu raia katika eneo la Fizi”

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, amafanya ziara Nchini Angola Jumapili, kwa lengo la kufufua mchakato wa Luanda, ukiwa mpango wa kidiplomasia unaolenga kurejesha amani mashariki mwa Kongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *