
Kufuatia mkutano wa wakuu wa nchi jijini Johannesburg mwezi uliopita, Marekani sasa inachukua urais wa G20 kwa mwaka 2026. Leo Jumatatu hii, Desemba 15,unafunguliwa mkutano wa kwanza wa G20 chini ya uenyekiti wa Marekani: mkutano wa Sherpas.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Valentin Hugues
Katika mkutano huu Afrika Kusini haitakuwepo: Rais Donald Trump hakutuma mwaliko Pretoria na hataki tena kuona Afrika Kusini ikishiriki vikao vya G20. Hata hivyo, Afrika Kusini inatumai kwamba kutengwa kwake kiholela katika mkutano huu wa kwanza kutakuwa miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo.
Hata ikiwa haipo, Pretoria inakusudia kupaza sauti yake. Serikali ya Afrika Kusini imetuma barua rasmi kwa nchi zote wanachama, ikiwaomba wafanye kutengwa huku kuwa mada kuu ya majadiliano katika mkutano huu wa kwanza.
Huu ni mkutano wa Sherpas, wawakilishi wa nchi za G20 waliopewa jukumu la kuanzisha mazungumzo sasa kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi, uliopangwa kufanyika mwaka ujao huko Miami. Hata hivyo, mwakilishi wa Afrika Kusini, Zane Dangor, hakupokea mwaliko. Hata hivyo, anabainisha kwamba hataingia kwa nguvu. “Sherpas wengine wote wanatuunga mkono,” aliongeza.
Mwanachama mwanzilishi wa G20
Donald Trump alisusia mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika Johannesburg mwezi uliopita. Rais wa Marekani aliuita mkutano huo kuwa “aibu,” akirejelea hadithi ya mauaji ya kimbari ya wazungu nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo, Afrika Kusini si mwanachama wa G20 tu: pia ni mmoja wa wanachama wake waanzilishi. Kwa hivyo, Washington haiwezi kuiondoa kwa muda mfupi tu.
Kuondoa nchi kutoka kwenye orodha kunahitaji makubaliano kati ya wanachama wote. Hali hii haiwezekani, kwani nchi kama Ujerumani na China tayari zimeonyesha uungaji mkono wao kwa Afrika Kusini.