#HABARI: Dunili Mageme Maduhu (56), mkazi wa kijiji cha Mwamugesha wilayani Itilima, amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na Hakimu Mkazi Mwandamizi Robert Kaanwa kwa kosa la kutishia kumuua baba yake mzazi, Abdalah Maduhu (90). Mgogoro huo ulizuka baada ya mzee huyo kumzuia mwanaye kuuza mali zake na mshtakiwa kujaribu kumfukuza mzazi wake katika nyumba anayomiliki, jambo lililopelekea mshtakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Kesi hiyo iliyosikilizwa Mahakamani hapo, upande wa Mashtaka uliita mashahidi wanne waliothibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo Oktoba 15, 2025, kinyume na kifungu cha 89 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Licha ya mshtakiwa kujitetea kwa kuleta mashahidi watatu waliodai alikuwa shereheni siku ya tukio, Mahakama ilitupilia mbali utetezi huo na kumtia hatiani baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu alizingatia ombi la upande wa mashtaka lililotaka adhabu kali itolewe ili iwe fundisho kwa jamii kukomesha vitendo vya kujichulia sheria mkononi na ukatili dhidi ya wazee. Hukumu hiyo inalenga kutoa funzo kwa watu wenye tabia ya kutishia uhai wa wazazi wao kwa sababu ya mali, ikisisitiza kuwa sheria itachukua mkondo wake kulinda kundi hilo la wazee.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *