Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) linaripoti kwamba mamia ya maelfu ya watoto na familia wanalazimika kukimbia wakitafuta hifadhi ndani ya DRC na nje ya nchi hususan nchini Burundi na Rwanda, kulingana taaria ya shirika hilo ya Desemba 13, 2025.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na UNICEF, tangu Desemba 1, mapigano makali yamesababisha zaidi ya watu 500,000, wakiwemo zaidi ya watoto 100,000 ndani ya Kivu Kusini pekee kuyahamamakazi yao. Kwa kuenea kwa vurugu, kuhama kwa watu kunatarajiwa kuongezeka zaidi. UNICEF imeelezea wasiwasi mkubwa kwa usalama na ustawi wa idadi kubwa ya watoto wanaokimbia na kutafuta hifadhi.

Onyo kwa pande zinazopigana

UNICEF inatoa wito kwa pande zote kuwalinda watoto na kuheshimu majukumu yao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na Mkataba wa Haki za Mtoto. Watoto hawapaswi kamwe kulipa gharama ya migogoro.

Mamia ya watu wameuawa tangu Desemba 2. Ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto pia umeripotiwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya wanafunzi wanne, wengine sita wamejeruhiwa, na mashambulizi katika angalau shule saba, huku madarasa yakibomolewa au kuharibiwa.

Kadri familia zinavyokimbia, watoto wanakabiliwa na hatari kubwa za ulinzi, ikiwa ni pamoja na kutengana na familia, kuathiriwa na vurugu, unyanyasaji wa kijinsia, utumwa, vurugu zinazotokana na jinsia, na dhiki ya kisaikolojia.

Majibu ya haraka wa kibinadamu

Wimbi kubwa la watu wanaokimbia vurugu umerekodiwa nchini Burundi. Kati ya Desemba 6 na 11, zaidi ya wageni 50,000 walitambuliwa, karibu nusu yao wakiwa watoto. UNICEF inatarajia idadi hii kuongezeka, hata hivyo, huku mamlaka zikiendelea kuwatambua wale wanaotafuta hifadhi.

Waliofika wengi wana majeraha yanayohusiana na migogoro. Zaidi ya hayo, pia kuna watoto wasio na wasindikizaji au waliotenganishwa, huku wanawake wakikabiliwa na hatari kubwa.

Hatimaye, UNICEF inahakikishia kwamba inafanya kazi na mamlaka za kitaifa na washirika nchini DRC na Burundi kuhamasisha mwitikio wa haraka wa kibinadamu unaozingatia watoto, huku ikishirikiana kwa karibu na mashirika na washirika wengine wa Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha tathmini za haraka na kuongezeka kwa msaada wa haraka iwezekanavyo hali ya usalama ikiruhusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *