
Watu thelathini na saba wamepoteza maisha siku ya Jumapili Desemba 14, huko Safi, kwenye pwani ya Atlantiki ya Morocco, kutokana na mafuriko ya ghafla kufuatia mvua kubwa iliyosababisha maji kuingia katika nyumba na maduka kadhaa. Hii ni idadi kubwa zaidi ya vifo kutokana na hali mbaya ya hewa nchini Morocco katika muongo mmoja.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Casablanca, Matthias Raynal
Nchini Morocco, mvua kubwa ilisababisha mafuriko mabaya mwishoni mchana wa Desemba 14, 2025. Maafa hayo yalikumba jiji la Safi, kwenye pwani ya Atlantiki, kilomita 250 kusini mwa mji wa Casablanca.
Kulingana na mamlaka katika eneo hilo, watu 37 walifariki. Hili ni janga baya zaidi la aina hiyo nchini Morocco katika angalau miaka 10.
Wakazi 300,000 wako katika hali ngumu kutokana na mafuriko hayo mabaya. Video zilizorekodiwa saa chache mapema zinaonyesha hali mbaya ya tukio hilo lililokumba jiji la bandari. Mvua kubwa ilinyesha katika mji wa Safi, na kusababisha mafuriko ya haraka na mabaya ndani ya saa moja tu, kulingana na mamlaka. Video zilizonaswa na wakazi zinaonyesha mitaa ikigeuzwa kuwa mito ya matope iliyojaa maji, ikisomba kila kitu kilichokuwa njiani.
Mbali na vifo hivyo, majeruhi pia yaliripotiwa, ikiwa ni pamoja na watu 32 waliopelekwa hospitalini, kulingana na mamlaka. Wengi wao wameruhusiwa kuondoka baada ya kupata huduma na matibabu yanayohitajika.
Mkazi aliyewasiliana na RFI ameelezea kwamba bonde, mto unaopita katikati ya jiji, ilivunja kingo zake. Medina maeneo ya zamani ya mji wa Safi, ndio yameathiriwa zaidi.
Jioni ya Jumapili jioni, kiwango cha maji kilikuwa tayari kimepungua, na kusababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na matope na magari yaliyopinduka. Vikosi vya usaidizi na ulinzi wa raia walikuwa wakifanya kazi ya kuondoa vifusi ambavyo bado vilisombwa na maji.
Utafutaji unaendelea kwa watu wowote ambao hawajulikani waliko, huku mamlaka zikifanya kazi ya kutoa msaada na usaidizi kwa watu walioathiriwa.
Kulingana na wakazi, idadi ya vifo bado inaweza kuongezeka.