Mamlaka imesema mvua kubwa ya usiku kucha ilisababisba mafuriko yaliosomba takriban nyumba 70 na biashara pamoja na magari 10. Mvua hiyo pia ilisababisha mafuriko na uharibifu katika maeneo mengine nchini humo ikiwa ni pamoja na mji wa Kaskazini wa Tetouan na ule wa milima wa Tinghir.

Video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii, zimeonyesha magari yakiwa yamekwama na sehemu kuzama huku mafuriuko hayo yakienea kwenye barabara za Safi.

Video nyingine iliyochapishwa na tovuti ya eneo hilo ya Safigoud.com imeonyesha mwanamke akivutwa baada ya kukwama katika maji ya mafuriko yenye tope mjini humo.

Mmoja wa manusura ambaye hakutajwa jina aliyezungumzia tukio hilo la jana, amesema mafuriko hayo yalianza mwendo wa alasiri.

”Tunashangaa kwa nini hakuna malori yaliokuja kuvuta maji, kama RADEES ambayo ni mamlaka ya usambazaji wa maji na umeme ya mkoa wa Safi ilivyokuwa ikifanya. Tunajua kwamba hili ni janga ambalo tunakubali kuwa linatoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wale waliohusika wako wapi?”

Mvua kubwa yanyesha Morocco baada ya ukame wa miaka saba

Morocco inashuhudia mvua kubwa na theluji kwenye milima ya Atlas baada ya miaka saba ya ukame uliochangia kukauka kwa mabwawa makuu ya maji.

Morocco Safi 2025 | Mafuriko
Viatu vilivyokwama kwenye tope la mafuriko mjini Safi nchini Morocco, Jumatatu Desemba 15,2025Picha: Abderrazak Gouach/AP Photo/picture alliance

Mafuriko ya wiki hii yametokea baada ya watu 22 kuuawa baada ya majengo mawili kuanguka katika mji wa Fez nchini humo.

Morocco imewekeza katika mipango ya kuzuia athari za majanga ingawa mara nyingi serikali za mitaa hazitekelezi kanuni za mifumo ya ujenzi na huenda mifumo ya mifereji ya maji ikakosekana katika baadhi ya miji.

Ukosefu wa usawa wa miundombinu ulikuwa lengo la maandamano yaliyoongozwa na vijana yalioikumba nchini hiyo mapema mwaka huu.

Mabadiliko ya hali ya hewa yachangia kutotabirika kwa hali ya hewa

Mabadiliko ya hali ya hewa yamefanya kuwa vigumu zaidi kutabirika kwa mifumo ya hali ya hewa.

Afrika Kaskazini imekumbwa na ukame wa miaka kadhaa, hali iliyosababisha udongo kuwa mgumu na kufanya milima, majangwa na maeneo tambarare kukabiliwa na athari zaidi ya mafuriko.

Mwaka jana, mafuriko katika maeneo ya kawaida ya milima na majangwa yalisababisha vifo vya takriban watu 12 nchini Morocco na Algeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *