
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anayehudhuria mkutano huo amesema nchi yake iko tayari kuachana na azma ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO ikiwa itahakikishiwa usalama wake, lakini Kiev imeshikilia msimamo wake wa kutoyaachia maeneo yake kwa Urusi.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani Stefan Kornelius amesema uthabiti wa makubaliano yoyote ya amani utategemea hakikisho la usalama litakalotolewa kwa Ukraine na kusisitiza kuwa maslahi ya bara zima la Ulaya yako hatarini na yanahitaji kulindwa. Kwa upande wake, ujumbe wa Marekani umeelezea kuridhishwa kwake na hatua zilizopigwa hadi sasa katika mazungumzo hayo.