Boti yenye kioo kinachomwezesha mtalii kutazama viumbe na baadhi ya vivutio vilivyo ndani ya maji, ijulikanao kama TAWA Sea Cruiser, imeendelea kuwa kivutio na kichocheo cha utalii wa ndani katika hifadhi ya magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, mkoani Lindi.
Afisa Utalii Kanda ya Kusini-Mashariki, Lembolos Ngengeya amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2025, matukio ya utalii zaidi ya 20 yamefanyika kupitia boti hiyo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi