Wakati Marekani ikiongeza shinikizo lake kwa Rwanda, ambayo inaunga mkono kundi la waasi, tangu Ijumaa, Desemba 12, AFC/M23 imetoa taarifa usiku wa Jumatatu, Desemba 15, kuamkia Jumanne, Desemba 16. Kundi hilo limetangaza kujiondoa kwa upande mmoja kutoka mji wa pili kwa ukubwa huko Kivu Kusini, kwa sharti la “kutokuepo na jeshi,” kwa mji huo, “ulinzi wa wa raia wake,” na “ufuatiliaji wa kusitisha mapigano kupitia kupelekwa kwa kikosi kisichoegemea upande wowote.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Chini ya wiki moja baada ya kuteka mji wa Uvira mashariki mwa DRC, AFC/M23 imetangaza kujiondoa kwa upande mmoja kutoka mji wa pili kwa ukubwa katika mkoa wa Kivu Kusini usiku wa Jumatatu, Desemba 15, kuamkia Jumanne, Desemba 16. “AFC/M23 itaondoa vikosi vyake kutoka mji wa Uvira kwa upande mmoja, kwa ombi la Marekani,” imeandikwa kwenye taarifa iliyochapishwa na kundi hilo la waasi. Ingawa M23 imeendelea kusonga mbele katika eneo hilo katika wiki za hivi karibuni, viongozi wake wanawasilisha uamuzi huu kama “kipimo cha kujenga imani katika kuunga mkono mchakato wa Doha.”

Hata hivyo, tangazo la kujiondoa huku linakuja na masharti. AFC/M23 inadai “kuondoa wanajeshi wote katika jiji la Uvira,” “ulinzi wa raia,” na “ufuatiliaji wa kusitisha mapigano kupitia kupelekwa kwa kikosi kisichoegemea upande wowote.”

Shinikizo la Marekani linaloongezeka kwa Rwanda

Hili pia linakuja wakati ambapo shinikizo la Washington kwa Rwanda, msaadizi mkuu wa AFC/M23, linazidi kuongezeka. Kufuatia kutekwa kwa mji wa Uvira wiki iliyopita, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, awali alisema mbele ya Baraza la Usalama siku ya Ijumaa, Desemba 12, kwamba Kigali “inaongoza eneo hilo kuelekea kutokuwa na utulivu mkubwa na kuelekea vita.”

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio aliendelea zaidi, akiishutumu Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya amani yaliyosainiwa mapema mwezi huu huko Washington chini ya usimamizi wa Donald Trump.

Hatimaye, siku ya Jumatatu, Desemba 15, kabla ya AFC/M23 kutoa taarifa yake, balozi wa Marekani nchini DRC, Lucy Tamlyn, alielezea kwamba nchi yake ilikuwa ikichunguza zana zote zilizopo—ikiwa ni pamoja na vikwazo—ili “kuhakikisha kwamba ahadi zilizotolewa zinaheshimiwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *