#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe, Bw. Olivanus Thomas, ameonyesha kukasirishwa na kusuasua kwa ukamilishwaji wa ujenzi wa majengo ya bwalo la chakula, mabweni mawili na vyoo vya wanafunzi, majengo yanayojengwa na wakandarasi wawili waliotambulika kwa majina ya Bw. Peter Nasokigwa na Bw. Kisha Muniru, ujenzi ambao unagharama zaidi ya shilingi milioni mia tano na ishirini ambapo kwa mujibu wa mkataba wanatakiwa kukamilisha miradi hiyo hapo Desemba 30 mwaka huu.
Bw. Olivanus Thomas ameonyesha kukerwa huko wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika shule hiyo ya Sekondari ya Njombe Techinical School shule ambayo inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi zaidi ya mia moja wa fani mbalimbali hapo January 16, 2026, ikiwa ni malengo ya serikali katika kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kundi la vijana kwa kuwapatia elimu ya sekondari yenye mchepuo wa ufundi wa fani mbalimbali ikiwemo ufundi umeme, uashi, seremala na tehama.
Bw. Olivanus ametoa maelekezo ya kukamilisha miradi hiyo haraka bila kuathiri kalenda ya masomo kwa wanafunzi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania