#HABARI: Mtu mmoja mwanamke mwenye umri wa miaka 36, anayejulikana kwa jina Agnes James, amefariki dunia huku wengine saba wakinusurika kifo kufuatia ajali ya moto, iliyotokea katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika Mtaa wa Mwasele “B”, Kata ya Kambarage, Manispaa ya Shinyanga.
Mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo Bw. David Johnson na jirani wa marehemu Mtitunga Mngata, wanasema moto huo ulianza ghafla na kusambaa kwa kasi hali iliyowafanya kushindwa kuokoa mali wala kuingia ndani ya nyumba.
Kwa upande wake Balozi wa Nyumba Kumi Bi. Rehema Shimiu pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwasele “B”, Bw. Cosmas Lucas, wamesema juhudi za pamoja na Jeshi la Zimamoto, hazikufanikiwa kuokoa maisha ya mama huyo kwa kuwa moto ulikuwa mkubwa uliokuwa unateketeza mali zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Wakati huo huo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, limesema chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyosababishwa na matumizi ya vyombo vingi vya umeme kwa wakati mmoja kwenye soketi za umeme huku likiwatahadharisha wananchi kuzingatia usalama wa vyombo vya moto majumbani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania