Jukwaa la Tuzo za Afya Barani Afrika limeiomba Serikali kuendelea kuimarisha huduma za afya vijijini, ikiwemo kuongeza idadi ya madaktari na wataalamu wa afya katika hospitali na vituo vya kutolea huduma, ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Africa Healthy Awards, Dkt. Abdallah Mshana, katika hafla ya utoaji wa tuzo za afya zilizolenga kutambua na kuthamini mchango wa hospitali na vituo mbalimbali vya afya nchini katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi