Nchini Kenya, watu wanaodaiwa kupatiwa kazi nchini Urusi wanaendelea kuajiriwa kwa nguvu kupigana kwa upande wa Urusi katika vita nchini Ukraine. Hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation, ambalo lilipata mfululizo wa mawasiliano ya kidiplomasia kati ya ubalozi wa Kenya huko Moscow na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix

Mark Kariuki alidhani amepata kazi katika usindikaji wa nyama nchini Urusi. Akiwa ameajiriwa na shirika lenye makao yake Nairobi, alilipa shilingi 30,000 pekee, sawa na chini ya euro 200, ili kupata visa ya Urusi katika wiki moja. Taratibu zote zilikamilishwa kupitia kikundi cha WhatsApp. Lakini alipofika Moscow, Mark alipelekwa kwenye kambi ya mafunzo ya kijeshi kabla ya kutumwa Ukraine.

Mafunzo ya haraka

Yeye ni mmoja wa Wakenya wachache walioandikishwa kwa nguvu katika jeshi la Urusi na kurejeshwa nyumbani na ubalozi wa Kenya. Kulingana na taarifa za kidiplomasia, zaidi ya wengine 80 bado wamekwama nchini Urusi, idadi ambayo huenda haithaminiwi, ubalozi unakiri. Kulingana na hati iliyosainiwa na Balozi Peter Mathuki, raia hawa wa Kenya walipelekwa kwenye kambi za mafunzo zilizoko Belgorod, Saint Petersburg, Rostov-on-Don, na Istra.

Huko Istra, kampuni ya kijeshi ya kibinafsi ya Wagner inasimamia kambi hiyo. Waajiriwa wengi wa Kenya ni raia, na wengine wamepitia mafunzo ya siku tano pekee. Mnamo mwezi Oktoba, waziri wa mambo ya nje wa Kenya alikutana na balozi wa Urusi jijini Nairobi, ambaye alimhakikishia kwamba hakuna wafanyakazi kutoka Kenya wanaolazimishwa kuajiriwa kwa nuvu katika jeshi la Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *