Lugha ya alama ni njia ya mawasiliano iliyobuniwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa kusikia.
Hata hivyo njia hii inatazamwa kama hitaji maalum kwa watu maalum na sio hitaji la msingi kwa watu wote hali inayowanyima fursa wanaoifahamu hususani wenye ulemavu wa kusikia ya kuwasiliana na jamii kwa mahitaji yote ya kijamii ikiwemo fursa za elimu, biashara na maisha ya kila siku.
Ili kutambua umuhimu wa jamii nzima kujifunza lugha hii, Ahmad Ally amezungumza na Amina Issah aliyepata changamoto ya kutosikia akiwa na umri wa miaka mitano.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi