MABADILIKO YA RATIBA ZA VIPINDI AZAM ONE KUANZIA JANUARI 2026

Msimamizi Msaidizi wa Chaneli ya #AzamONE, @kechu_jackson ameeleza kuhusu mabadiliko ambayo chaneli hiyo inaenda kuyafanya kuanzia Januari mosi 2026.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni ratiba za vipindi ambayo yatahusisha, ratiba ya tamthilia za saa 3:00 usiku na saa 4;00 usiku, ambazo zitakuwa zikiruka Jumatatu hadi Alhamisi, huku ratiba ya saa 1:00 usiku ikibaki kama ilivyo Jumatatu hadi Ijumaa.

Pamoja na mabadiliko hayo, tamthilia kali kama Grey’s Anatomy na Marvel’s #ThePunisher zitapamba msimu wako wa sikukuu, huku vipindi bomba kama #MasterChef na America’s Got Talent vikikuacha na tabasamu muda wote.

Hii ndio maana halisi ya tumuifungua AzamONE, tumefungua kufuli la burudani.

#AzamONEUnloacked

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *