Balozi wa Marekani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lucy Tamlyn, ameelezea kujitolea kwa nchi yake kutekeleza Mkataba wa Amani wa Washington, uliosainiwa kati ya DRC na Rwanda.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Marekani nchini DRC, alitoa kauli hii katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu hii, Desemba 15, huko Kinshasa:

“Tunachunguza zana zote zinazowezekana za kidiplomasia, vikwazo, pamoja na shughuli za pande mbili na za kimataifa ili kuhakikisha kwamba ahadi zilizotolewa zinaheshimiwa.”

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani pia alielezea kukatishwa tamaa kwa nchi yake na kuibuka tena kwa vurugu mashariki mwa DRC, ambazo zilitokea siku moja baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Washington, akiishtumu Rwanda ka kuhusika katika vurugu hizo.

Kulingana na Lucy Tamlyn, kuanguka kwa jiji la Uvira, mji mkuu wa muda wa mkoa wa Kivu Kusini, hakumaanishi kushindwa kwa utawala wa Trump, ambao ulifadhili makubaliano haya.

“Nadhani Rais Trump ameonyesha kwamba anataka kupigania amani nchini DRC. Yeye mwenyewe amejitolea sana na anafuatilia hali ilivyo kwa maslahi makubwa,” alibainisha.

Kupitia balozi wao, Marekani ilituma ujumbe wa amani na matumaini kwa raia wa Kongo, wakati ambapo jiji la Uvira limeangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Desemba 11, na msemaji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alilaani vikali shambulio jipya lililoanzishwa na waasi wa AFC/M23 katika maeneo kadhaa katika moa wa Kivu Kusini, ikiwa ni pamoja na Kamanyola, Luvungi, Katogota, na Uvira, ambalo lilisababisha vifo vya raia.

Katibu Mkuu anatoa wito wa kukomeshwa kwa uhasama mara moja na bila masharti, kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama nambari 2773 (2025). Anaonya kwamba ongezeko hili la mapigano linahatarisha kudhoofisha juhudi za kufikia suluhisho la kudumu la mgogoro huo na kuongeza hatari ya mapigano makubwa ya kikanda. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *