Fedha hizo, ambazo ni sawa na takribani dola milioni sita za Kimarekani, zilikamatwa ikiwa ni wiki tatu tu tangu mapinduzi ya kijeshi kwenye taifa hilo la pwani ya Afrika Magharibi.

Mtu huyo alishikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Figo Maduro siku ya Jumapili (Disemba 14) lakini akaachiwa kwa dhamana siku ya Jumatatu, kwa kuwa chini ya sheria za Ureno, adhabu ya kosa alilokamatiwa haizidi kifungo cha miaka mitano jela.

Idara ya Mwendesha Mashitaka haikuweka hadharani jina la mshukiwa huyo, ingawa vyombo vya habari vya Ureno vimemtaja kama mpambe wa Embalo, na kwamba alikamatwa akiwa kwenye ndege moja na mke wa rais huyo wa zamani, ingawa mke huyo hakutiwa kizuizini.

Embalo alipinduliwa na jeshi baada ya uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi Novemba, ambao upinzani unasema ulishinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *