Rais Donald Trump wa Marekani amelifungulia mashtaka Shirika la Habari la BBC kwa kukiuka maadili ya taaluma ya uandishi wa habari kwa kuhariri (kwa namna ya upotoshaji) vipande vya hotuba yake na kuifanya itafsiriwe kuwa aliwachochea wafuasi wake kuvamia na kufanya uharibifu katika jengo la Bunge la Marekani ‘Capitol’.

Trump amefungua mashtaka hayo akitaka kulipa fidia ya mabilioni ya Dola za Marekani kwa alichokidai “kuchafuliwa jina”.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *