Dar es Salaam. Wachezaji Jonathan Sowah na Allasane Kante wamefungiwa kucheza mechi tano kila mmoja kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu waliyofanya dhidi ya Azam FC, Desemba 7, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania leo, imeeleza kuwa refa wa mchezo huo, Abdallah Mwinyimkuu pia amefungiwa mizunguko mitano kwa kushindwa kuchezesha vizuri mechi hiyo.

Mbali na kufungiwa, wachezaji hao kila mmoja ametozwa faini ya Sh1 milioni.

“Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:21 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji,” imefafanua taarifa hiyo.

Refa wa mechi hiyo, Abdallah Mwinyimkuu kutoka Singida, yeye ameondolewa kuchezesha katika mizunguko mitano ya Ligi Kuu kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria za soka.

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh5 milioni kwa kosa l shabiki wake kuingia katika eneo la kuchezea kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union.

Katika hatua nyingine, kiungo wa Singida Black Stars, Khalid Aucho naye amefungiwa mechi tano na faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tabora United.

Refa wa mechi hiyo, Alex Pancras yeye amepewa onyo kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *