Katifa taarifa, mkuu wa IRC  David Miliband , amesema kile shirika hilo limekiona kwenye mitaa na vijiji vya nchi hiyo siyo jambo la bahati mbaya na kwamba ulimwengu haushindwi kushughulikia tu mzozo huo bali matendo na maneno yanarefusha na kuuzawadia mzozo huo.

Miliband amesema ukubwa wa mgogoro nchini Sudan, unaoshikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya shirika hilo kwa mwaka wa tatu mfululizo na ambao sasa ndio mgogoro mkubwa zaidi kurekodiwa, ni ishara ya mparaganyiko unaoshuhudiwa kote ulimwenguni.

Orodha hiyo inaangazia nchi 20 ambazo zinakabiliwa na hatari zaidi ya dharura mpya au mbaya zaidi za kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *