Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Thailand Maratee Nalita Andamo, amewaambia waandishi wa habari mjini Bangkok kwamba kama mwanzilishi wa vurugu hizo katika ardhi ya Thailand, lazima Cambodia iwe ya kwanza kutangaza amani.

Cambodia haikujibu mara moja taarifa hiyo ya Thailand.

Mapigano mapya kati ya mataifa hayo mawili jirani ya kusini-mashariki mwa Asia mwezi huu yamesababisha vifo vya takriban watu 32, wakiwemo wanajeshi na raia, na kuwafanya takriban watu 800,000, kuyakimbia makazi yao.

Kila upande umelaumu mwingine kwa kuanzisha mapigano hayo, ukidai kujilinda na kudai mashambulizi dhidi ya raia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *