
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amekutana na mjumbe wa Marekani Steve Witkoff, kujadili mapendekezo ya rais Donald Trump kuhusu kumaliza vita kati ya Ukraine na Urusi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mjumbe huyo wa Trump, kupitia ukurasa wake wa X, amesema, hatua kubwa imepigwa kuanzia Jumapili baada ya kuanza kwa mazungumzo hayo jijini Berlin nchini Ujerumani.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea siku ya Jumatatu, ripoti kutoka ndani zimesema, Marekani bado inaitaka Ukraine kukubali vikosi vya Urusi kudhibiti eneo la jimbo la Donbas, kama sharti muhimu la kupata mwafaka.
Hata hivyo, pendekezo hili linapingwa vikali na Ukraine, huku kiongozi wake, Zelenksky baadaye leo jioni akitarajiwa kukutana na wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya na NATO kwa ajili ya majadiliano zaidi.
Rais Trump amekuja na mapendekezo 28 yanayoonekana kuipendelea zaidi Urusi, kwenye mchakato huo wa kupata amani, huku Ukraine ikisema iko tayari kuachana na mpango wake kuwa mwanachama wa NATO iwapo itapata hakikisho la kiusalama.