Viongozi wa mataifa 34 na Ukraine wamekubaliana rasmi mipango ya kuunda chombo maalumu cha kusimamia mchakato wa kuilipa fidia Ukraine kwa fedha za Urusi.

Mpaka hivi sasa viongozi wa Ulaya wanakubaliana kwamba Ukraine inapaswa kulipwa fidia ya uharibifu uliosababishwa na vita vya Urusi. Lakini suala kubwa linaloulizwa ni, wapi zitakakotoka fedha hizo.

Baraza la Ulaya linashikilia kwamba Urusi inapaswa kufadhili gharama za uharifu uliofanyika ndani ya Ukraine, japokuwa bado hakuna namna ya wazi iliyofikiwa ya kuilazimisha Moscow kuchukuwa jukumu hilo.

Mkutano wa wajumbe wa Marekani na Ulaya kujadili hali ya Ukraine mjini Berlin
Ulaya inakubaliana kwamba Ukraine inapaswa kulipwa fidia ya uharibifu uliosababishwa na vita vya UrusiPicha: Guido Bergmann/Handout Bundesregierung/dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Mojawapo ya mapendekezo yaliyotolewa ni kutumika sehemu ya mabilioni ya dolla za Urusi zinazozuiwa kwenye mataifa ya Ulaya. Michael McGrath Kamisha wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya demokrasia na haki akiunga mkono fikra hiyo: “Hatutazami kando kuona namna nyingine ya Urusi inavyokimbia kuchukuwa dhamana na kutokuwa tayari kulipa, kwasababu kwa mtazamo wangu hilo litakuwa tu linawapa nafasi nyingine ya kukwepa jukumu lao”

Rais Volodymyr Zelensky amewaambia viongozi waliokusanyika The Hague nchini Uholanzi kwamba ana matarajio ya kupata uungwaji mkono mkubwa  wa kimataifa kwenye suala zima la nchi yake kulipwa fidia ya uharibifu uliotokana na vita hivyo vya Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz katika kikao cha waandishi habari
Ukraine inazitaka nchi za Ulaya ziridhie matumizi ya mali za Urusi katika kuijenga upya nchi hiyoPicha: Halil Sagirkaya/Anadolu Agency/IMAGO

Zelensky amesisitiza kwenye mkutano huo kwamba nchi yake inakabiliwa na matatizo  na kwahivyo uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuridhia mali za Urusi zinazozuiliwa katika mataifa ya kanda hiyo zitumike kwaajili ya kuisadia nchi yake ni muhimu. “Shinikizo dhidi ya Urusi ni lazima liendelee, mradi bado nchi hiyo inaendelea kukalia ardhi yetu.

Urusi inapaswa kujihisi kwamba ni mhalifu na kuzikabili athari zinazomuandama, ikiwa bado watu wetu wanaendelea kushikiliwa mateka na nchi hiyo. Na hadi pale watoto wa Ukraine waliotekwa nyara na Urusi watakaporejeshwa nyumbani .Vikwazo vinabidi kuendelea kuikabili Urusi mpaka itakapoheshimu maisha ya amani  na haki ya majirani zake.”

Rais Zelensky amebaini kwenye mkutano huo kwamba haoni fursa ya taifa lake kusimama imara dhidi ya Urusi bila ya uungaji mkono wa mataifa hayo.

Amewaambia viongozi wa Ulaya kwamba kutumiwa mali za Urusi zinazozuiliwa kwenye mataifa hayo kutaisadia Kiev kuweka urari kwenye pengo la msaada uliopunguwa kutoka kwa baadhi ya washirika wake. Lakini wakati viongozi hao wa Ulaya wakihangaika kutafuta namna ya kuendelea kuiunga mkono Ukraine, Urusi imetangaza kulikataa pendekezo la usitishaji vita nchini Ukraine katika kipindi cha sikukuu ya Xmas.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitri Peskow
Urusi imetangaza kulikataa pendekezo la usitishaji vita nchini Ukraine katika kipindi cha sikukuu ya XmasPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/ZUMA/picture alliance

Msimamo huo wa Kremlin umetolewa baada ya Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz Jana Jumatatu kumtolea mwito rais Vladmir Putin kusimamisha mapigano wakati wa sikukuu hiyo.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amenukuliwa akisema kwamba Moscow inataka amani na haina haja na usitishaji wa muda wa mapigano. Urusi inaamini kwamba usitishaji mapigano kipindi cha Krismasi, utaipa fursa Ukraine kujipanga upya na kujiandaa kuendelea na vita. Wito wa Merz aliutowa baada ya mkutano uliofanyika Berlin kwa siku mbili kati ya Ukraine Ulaya na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *