Umoja wa Mataifa unataka kuachiwa bila kwa masharti kwa watu wanaokadiriwa kuwa Elfu 10, waliokamatwa na kuzuiwa nchini Eritrea, wakiwemo wanasiasa, wanahabari na wanafunzi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Seif Magango, msemaji wa Ofisi ya Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za binadamu, amesema watu hao wanapswa kuachiwa haraka, kama ilivyokuwa kwa wengine 13 walioachiwa hivi karibuni, baada ya kuzuiwa kwa karibu miaka 18.

Umoja wa Mataifa unasema, kundi la waliokuwa maafisa wakuu serikali wanaojitta G11 waliofungwa mwaka 2001 kwa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uongozi nchini humo, wanapaswa kuachiwa huru.

Aidha, Umoja wa Mataifa unasema, uko tayari kushirikiana na uongozi wa Eritrea kuhakikisha kuwa, inaheshimu na haki za binadamu kwa mujibu wa mikataba ya Kimataifa.

Wito huu unakuja, katika nchi hiyo inayoongozwa na kiongozi wa muda mrefu Isaias Afwerki, ambaye amekuwa madarakani, tangu mwaka 1993, aliye na rekodi ya kutovumilia ukosoaji kuhusu utawala wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *