
Katika taarifa, shirika hilo limesema haliwezi kuweka mifumo thabiti ya kukabiliana na msimu wa baridi wakati pia likiongeza msaada wake wa dharura na lishe kote duniani.
WFP imesema inahitaji zaidi ya dola milioni 460 kutoa msaada wa chakula kwa Waafghanistan milioni 6 walio hatarini zaidi.
Taarifa hiyo pia imesema vifo vya watoto huenda vikaongezeka wakati wa miezi ya baridi kali nchini Afghanistan wakati kuna uhaba mkubwa zaidi wa chakula.
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula na Uangalizi wa Lishe wa shirika hilo la WFP, Jean-Martin Bauer, amewaambia waandishi wa habari huko Geneva kwamba wanaufadhili wa asilimia 12 pekee na hicho ni kikwazo.