
Ni mambo ya bata batani! Wazungu wanasema ‘December to remember’ ndivyo ambavyo msemo huu hutamkwa ukimaanisha ni muda wa kujenga kumbukumbu mbalimbali kwani ni mwezi ambao ndugu jamaa na marafiki hukutana kwa pamoja kufurahia likizo na kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Watu hurudi makwao kwa ajili ya kusherehekea na familia kwa kunywa, kula na kusaza. Kati ya mikoa ambayo hupokea wageni wengi ni Kilimanjaro. Hivyo basi hizi hapa sehemu tisa za kujidai rikizo hii ukiwa Kiilimanjaro.
Kwa wale wa Njiapanda ya Moshi Mjini/Himo yapo machaka mengi ya kujificha lakini hakikisha haukosi kutembelea machimbo haya.
D.I.D ukale bata kisha kabla kabla hujaondoka Njiapanda sogea Mombasa Highway hapo utapata nyama choma za uhakika bila kusahau vinjwaji vya kibabe.
Ukiingia tuu Moshi Mjini hapo ndipo kuna viwanja vya kutosha hivyo kabla hujamaliza likizo tembelea Moshi Pazuri Bar & Restaurant iliyoko maeneo ya YMCA hapa kuna BBQ, Live Music, Food, Drink kwa kifupi kuna vibe la kutosha usiondoke kabla hujafika hapa.
Delight hii pia ipo maeneo ya YMCA jirani kabisa na Moshi Pazuri wazee wa kukesha hili ndilo eneo lao. Siyo vibaya ukaanzia maeneo mengine kisha ukaenda kukesha Delight.
Eneo hili ni zuri zaidi ukienda ukiwa tayari umechangamka ili uweze kuendana na vibe lake maana pamechangamka si mchezo.
Unaachaje kufika Kill East hili chimbo lipo Moshi mjini maeneo ya Mjohoroni Mdawi hapa ni vibe juu ya vibe wale wa kuwaka vyombo vipo vya kutosha moja moto moja baridi.
Nyama choma za kibabe utazipata ‘Kwa Mambo’ maeneo ya Rau KCMC. Hata Garden Bar pia wapo vizuri sana kwenye uchomaji wa nyama hawa utawapata Forest kwa Alfonsi.
Hakikisha haurudi ulipotoka bila kuwa na kumbukumbu ya Hugoss na Red Stone haya ni machimbo mawili tofauti lakini vibe lake usipime mtu wangu usipofika hapa jihesabie bado haujala bata Moshi. Sehemu hizi zote mbili zipo Moshi Town.
Majengo Min Koboriloni nako hapako kinyonge kuna 80 Pub hii balaa chukua washikaji nendeni mkajichimbie huku. Wale wa KCMC Mapipa kapondeni raha Amuz au Mimiz. Uliza wenyeji watakupeleka.