Katika taarifa yake iliyochapishwa usiku wa kuamkia leo, kundi la AFC/M23 limetangaza kwamba litaondoa vikosi vyake kutoka mji wa Uvira, kuitikia ombi la Marekani. Viongozi wa AFC/M23 wanadai kwamba uamuzi huo ni mojawapo ya hatua za kujenga imani katika kuunga mkono mchakato wa amani wa mjini Doha, Qatar.
AFC/M23 inasisitiza kwamba imekusudia kujiondoa huko chini ya masharti matatu ikiwa ni pamoja na kutokuwepo askari mjini Uvira, ulinzi wa wakazi na ufuatiliaji wa usitishaji mapigano kupitia kutumwa kwa jeshi lisiloegemea upande wowote. Caleb ni Mkazi wa Uvira, pamoja nakupongeza hatuwa hiyo ya AFC.M23, bado ana masito.,
Haya yanajiri wakati shinikizo la Washington kwa nchi ya Rwanda inayodaiwa kuunga mkono AFC/M23, likiongezeka. Kufuatia kutekwa kwa mji wa Uvira wiki iliyopita, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, awali alisema mbele ya Baraza la Usalama Ijumaa iliopita kwamba serikali mjini Kigali inaongoza eneo la mashariki mwa Kongo kuelekea vita.
Wikiendi hii iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio aliituhumu Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mapema mwezi huu mjini Washington chini ya mwamvuli wa Donald Trump.
Jean-Chrysostome Kijana, mwanachama wa mtandao wa mashirika ya kiraia uitwao Pamoja Kwa Amani, anaamini kuwa hatuwa ya AFC/M23 ni njia ya kuvuruga Umoja wa Mataifa, hasa kwa vile AFC/M23 tayari ilikuwa imesonga mbele zaidi ya Uvira.
Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Chama cha PPRD cha Rais Wazamani Joseph Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary, alikamatwa mjini Kinshasa usiku wakuamkia leo nyumbani kwake na watu wenye silaha ambao baadhi yao walikuwa wamevalia kiraia na kupelekwa kusikojulikana. Chama chake kinadai aachiliwe huru.