
Hapo jana, takriban washtakiwa 30 walifikishwa mbele ya mwendesha mashtaka maalum wa mahakama ya uhalifu wa kiuchumi na ugaidi mjini Cotonou na kuwekwa kizuizini kabla ya kuanza kusikizwa kwa kesi hiyo leo.
Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa watu hao wanashtakiwa kwa uhaini, mauaji na kuhatarisha usalama wa taifa.
Katika hatua nyingine, Chabi Yayi, mtoto wa rais wa zamani wa Benin na kiongozi wa sasa wa upinzani Thomas Boni Yayi, aliachiliwa jana baada ya kuhojiwa.
Hata hivyo, bado anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na jaribio hilo la mapinduzi kwa sababu ambazo hazijulikani huku mamlaka ikizidi kuwahoji viongozi wa upinzani.