Akiandika katika Ukurasa wake wa X, Bizimana amesema kile M23 inachofanya ni kuonesha Rwanda inajaribu tu kupunguza shinikizo la kimataifa.

Rwanda imeendelea kukanusha kwamba inalipa msaada wa kijeshi kundi hilo na kushinikiza kuwa inakabiliwa na kitisho cha usalama kutoka kwa wanamgambo wa Kihutu walioko mashariki mwa Kongo, wanaofungamanishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.

Hata hivyo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasisitiza kuwa Rwanda imekuwa na jukumu muhimu katika kuwasaidia waasi hao.

Wiki iliyopita, waasi wa M23 walichukuwa udhibiti wa mji wa kimkakati wa Uvira, ulioko karibu na mpaka wa Burundi, siku chache baada ya serikali za Kongo na Rwanda kusaini mkataba wa amani mjini Washington, Marekani.

  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *