CHINA YAPUNGUZA USHURU WA NYAMA YA NGURUWE YA ULAYA
#HABARI: China imepunguza ushuru wa uangizaji wa nyama ya nguruwe kutoka Umoja wa Ulaya, hatua iliyoanza kutekelezwa leo.
Wizara ya Biashara ya China imesema kiwango cha juu cha ushuru kwa nyama ya nguruwe ya Ulaya kitakuwa chini ya asilimia ishirini, kiwango ambacho ni chini ya theluthi moja ya ushuru uliowekwa mwezi Septemba.
Hatua hiyo imepokelewa kwa ahueni na wazalishaji wa nyama ya nguruwe barani Ulaya, hasa nchini Hispania na Ufaransa.
China ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kula nyama ya nguruwe; mnamo 2024, zaidi ya nusu ya uagizaji wake wa thamani ya dola za Marekani bilioni 4.8 ulitoka Umoja wa Ulaya.
Wakulima wengi wa Ulaya wanategemea sana soko la China, hasa ikiwa kwamba utumbo wa nguruwe, masikio na miguu ya nguruwe haviliwi sana katika maeneo mengine ya dunia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.