Rais wa Marekani Donald Trump, siku ya Jumanne Desemba 16 amepanua orodha ya raia wa kigeni waliopigwa marufuku kuingia nchini Marekani, ambayo sasa inajumuisha Raia wa Syria, Burkina Faso, Mali, na Palestina. Marufuku ya awali ya usafiri “travel ban”, iliyotangazwa mwezi Juni, iliwalenga raia wa Nchi 12.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump ameongeza majina mengine kwenye orodha yake ya nchi zisizohitajika. Rais wa Marekani, siku ya Jumanne, Desemba 16, ameongeza marufuku ya kuingia Marekani kwa raia wa mataifa mengine saba, ikiwa ni pamoja na Syria, pamoja na Wapalestina, Ikulu ya White House imetangaza.

Rais Trump “amesaini tu tangazo linalozuia na kupunguza kuingia kwa raia wa kigeni ili kulinda usalama wa Marekani,” Ikulu ya White House imesema kwenye moja ya kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Nchi nyngine zilizoathiriwa na marufuku ya jumla ni Burkina Faso, Niger, Mali, Sudan Kusini, na Syria, huku nchi zingine mbili, Laos na Sierra Leone, zimejikuta zikitoka kwenye vikwazo vya sehemu hadi jumla, kulingana na tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump.

Wapalestina walio na hati za kusafiri zilizotolewa na Mamlaka ya Palestina pia wanalengwa.

Kuhusu Syria, hatua hiyo inakuja siku chache baada ya shambulio baya dhidi ya wanajeshi wa Marekani katikati mwa nchi.

Vighairi, haswa kwa watu ambao “kiingilio chao kinaendana na maslahi ya kitaifa”

Utawala wa Trump unasema umetambua nchi ambazo uchunguzi “hautoshi sana kiasi kwamba ulihitaji kusitishwa kabisa au kwa sehemu kwa raia wa nchi hizo.”

Hata hivyo, tangazo hilo linajumuisha vighairi kwa wakazi halali wa kudumu, wamiliki wa visa waliopo, aina fulani za visa kama vile wanariadha na wanadiplomasia, na watu binafsi ambao “kiingilio chao kinaendana na maslahi ya kitaifa ya Marekani.”

Tangu arejee madarakani mwezi Januari, Donald Trump amekuwa akiendesha kampeni pana dhidi ya uhamiaji haramu na ameimarisha kwa kiasi kikubwa mahitaji ya kuingia Marekani na utoaji wa visa, akitaja hitaji la kulinda usalama wa taifa.

Hatua hizi zinalenga kuzuia kuingia Marekani kwa wageni ambao “wanakusudia kuwatishia” Wamarekani, kulingana na Ikulu ya White House. Vile vile, zinalenga wageni ambao “wanaweza kuharibu utamaduni, serikali, taasisi, au kanuni za msingi” za Marekani.

Hivi majuzi rais wa Marekani alizindua shambulio kali dhidi ya Wasomali, akisema “hawataki nchini Marekani.”

Mnamo mwezi Juni, alitangaza marufuku ya kuingia Marekani kwa raia wa nchi kumi na mbili, hasa barani Afrika na Mashariki ya Kati (Afghanistan, Burma, Chad, Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan, na Yemen).

Kwa upande mwingine, Turkmenistan, moja ya nchi zilizotengwa zaidi duniani, imepongezwa na Marekani, huku Ikulu ya White House, siku ya Jumanne, ikitaja “maendeleo makubwa” katika taifa hili la Asia ya Kati. Kwa hivyo, raia wa Turkmenistan wataweza tena kupata visa vya Marekani, lakini tu kama wasio wahamiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *