‎#HABARI: Wananchi wa Jiji la Mbeya wameelezea kutoridhishwa kwao na kitendo cha kubambikiwa ankara kubwa za maji ambazo haziendani na matumizi yao halisi, hali inayotajwa kusababishwa na makosa ya kitaalamu kutoka kwa watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (UWSA). Kilio hicho kimefikishwa mbele ya Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa haraka utakaowawezesha wananchi, hususan wenye kipato cha chini, kulipa gharama halisi na za haki.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mhe. Patrick Mwalunenge, amethibitisha kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu adha hiyo ya madeni yasiyo na uhalisia. Mhe. Mwalunenge ameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo ili kuondoa mzigo wa gharama unaowaumiza wakazi wa Mbeya na kuhakikisha kuwa makosa yanayofanywa na wataalamu wa mamlaka ya maji yanarekebishwa mara moja.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, baada ya kusikiliza hoja na malalamiko hayo, ametoa ahadi ya kulishughulikia suala hilo kwa uzito wa juu. Amesema kuwa wizara itafuatilia kwa karibu utendaji wa Mbeya UWSA ili kuondoa changamoto hiyo ya ankara zisizo na uhalisia na kuhakikisha kuwa huduma ya maji inatolewa kwa uadilifu na uwazi kwa wananchi wote.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *