#HABARI: Wananchi zaidi ya 1062 wa Kijiji cha Makunda, wilayani Iramba, mkoani Singida, walioomba kupatiwa hati miliki za kimila zaidi ya miaka mitatu iliyopita, hatimaye wamepatiwa hati hizo kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi unao simamiwa na Wizara ya Ardhi, ambapo zinatajwa kuwa msaada mkubwa kwenye kutatua migogoro ya ardhi na kupata mikopo mbalimbali ikiwemo ya kilimo.
Wakizungumzia hatua hiyo wananchi hao huku wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kukabidhiwa hati hizo, wanaeleza jinsi walivyo kuwa wakizisubiri kwa muda mrefu na zitakavyo wasaidia kwenye kupunguza migogoro ya ardhi na dhamana ya kupata mikopo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania.