#HABARI: Watahiniwa 4,414 wa tasnia za Uuguzi na Ukunga nchini, wanaotarajia kufanya mtihani wa usajili na leseni wa Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC), wamehasishwa kujiepusha na tabia za udanganyifu kabla ya mtihani, wakiwa chumba cha mtihani na hata baada ya mtihani kwani wakibainika na udanganyifu wa aina yoyote, adhabu yake ni kufutiwa mtihani kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukuga.
Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari jijini Dodoma, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Tanzania Bi. Agnes Mtawa, ametanabaisha kuwa, Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010 kifungu cha 19(3) pamoja na kanuni yake kifungu cha 22, kinabainisha adhabu ya kufutiwa mtihani kwa mtahiniwa yeyote atakayetenda kosa la udanganyifu.
Ameongeza kuwa, jukumu hili la kuendesha mitihani ya kupima umahiri kwa wahitimu wa vyuo wa taaluma hizo mbili, linafanyika ili kuhakikisha umma unapata huduma iliyobora na salama za uuguzi na ukunga kutoka kwa wataalamu wenye weledi na umahiri kabla ya kusajiliwa rasmi na kupewa leseni za kuwatambua.
Aidha, watahiniwa wametakiwa kufika katika vituo vyao kwa wakati na vifaa muhimu ambavyo ni Kalamu Nyeusi (aina ya Obama) au Penseli (HB Orginal) Picha mbili (passport size) Kitambulisho (Indexing card) kwa wale wasiokuwa na Indexing kadi wanatakiwa kuja na moja kati ya vitambulisho vifuatavyo; Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kitambulisho cha Mpigakura au Leseni ya udereva na wakiwa nadhifu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania.