Ubalozi wa Israel nchini Canada, umesema Israel imechukua hatua hiyo, kutokana na ujumbe huo kudaiwa kufungamana na shirika lisilokuwa la kiserikali la Islamic Relief Worldwide, ambalo Israel imeliorodhesha kama shirika la kigaidi.

Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Canada Anita Anand, amesema katika mtandao mmoja wa kijamii kwamba nchi yake imeelezea kupinga namna raia wake walivyohangaishwa.

Iqra Khalid, mmoja ya wabunge anayetokea chama cha Kiliberali cha Waziri Mkuu Mark Carney, amesema alikuwa sehemu ya ujumbe huo na alisukumwa mara kadhaa na maafisa wa jeshi la Israel.

Ujumbe huo ulipanga kukutana na Wapalestina waliopoteza makaazi yao katika Ukingo wa Magharibi, ambako serikali ya Israel hivi karibuni iliidhinisha ujenzi wa nyumba mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *