Ikiwa na idadi ya watu milioni 100, Ethiopia ndiyo nchi ambayo haina bandari na yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Waziri Mkuu Abiy Ahmed ameweka wazimu nia yake ya kupata kufikia Bahari ya Shamu, ambayo Ethiopia ilipoteza wakati walipotengana na Eritrea 1993. Serikali yake inasisitiza kuwa inataka kutumia bandari hiyo kwa amani.

Wataalamu wanalaumu kuongezeka kwa uhasama kwa matumizi ya bandari kutokana na kufeli kwa dilplomasia na changamoto katika Jumuiya za kikanda.

“Kilichoandikwa na kinachofanyika ni vitu viwili tofauti. Inapokuja suala la utekelezaji, au sehemu ya utekelezaji au maslahi binafsi yanajitokeza. Hili ni suala ambalo linaathiri nchi nyingi ambazo hazina bandari katika kanda,” Profesa David Mugisha, Mwanazuoni wa masuala ya uhusiano wa kimataifa, ameiambia TRT Afrika.

Jaribio la Ethiopia Januari 2024 kutaka kukodi kilomita 20 ya mwambao wa pwani kutoka kwa eneo lililojitenga la Somaliland lilizua taharuki ya kidiplomasia, huku Somalia ikishtumu Ethiopia kwa kudharau uhuru wa mpaka wake.

Juhudi za Uturuki za kuleta upatanishi ziliweka msingi wa kuleta amani kati ya mataifa hayo mawili jirani, kuelekea kupatikana kwa kile kilichojulikana kama Azimio la Ankara ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia walikubaliana kuheshimu uhuru wa mataifa yao.

Hata hivyo, Abiy anaendelea kuonesha nia ya kuwa na bandari ya bahari. Aliwaambia wabunge wa Ethiopia mwezi Oktoba kuwa “ana uhakika asilimia milioni moja” Ethiopia haitobaki kuwa nchi isiyo na bandari daima, “iwe mtu anataka au hataki”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *