
Dar es Salaam. Katika mwendelezo wa Sera za Rais wa Marekani, Donald Trump katika kuzidisha vikwazo kwa wahamiaji nchini humo, Marekani imeondoa viza kwa mataifa mengine 15, ikiwamo Tanzania kuzuiwa kuingia nchini humo.
Zuio hilo limelenga makundi yaliyoainishwa na Taifa hilo yakiwamo viza B-1 inayohusu wageni wa kibiashara, viza B-2 inayohusu wageni wa kutalii, viza- F inayohusu wageni wanafunzi wa kitaaluma, viza- M inayohusu wanafunzi wa ufundi wa masomo yasiyo ya kitaaluma na viza – J inayohusu wageni wa kubadilishana uzoefu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani, sababu ya kuzia makundi kadhaa ya viza ni kutokana na waombaji kupitiliza muda wa ruhusa iliyotolewa na ‘kuzamia.’
Kwa upande wa Tanzania, taarifa ya Ikulu ya Marekani imebainisha kuwa waliozamia kwa kuzidisha muda wa ruhusa iliyotolewa kwenye viza imezidi hadi asilimia 8.30 kwa wahamiaji wa makundi ya viza ya B-1 na B-2 huku kwa makundi ya viza F, M na J wakifikia asilimia 13. 97.
Pia, mataifa mengine yaliyoondolewa viza za kwenda katika Taifa hilo tajiri ulimwenguni ni Angola, AntiguAa, Barbuda, Benini, Ivory Coast, Dominica, Gabon, Gambia, Malawi, Mauritania, Nigeria, Senegal, Tonga, Zambia na Zimbabwe.
Marekani imesema kuondolewa kwa viza kwa mataifa hayo ni juhudi za Taifa hilo kuimarisha ulinzi na usalama ikitaja kuwa wahamiaji wengi wanapoingia Marekani wanazamia kwa muda mrefu bila kurudi katika mataifa yao.
Marekani imesema kuondolewa kwa viza kwa mataifa hayo ni juhudi za Taifa hilo kuimarisha ulinzi na usalama ikitaja kuwa, wahamiaji wengi wanapoingia katika Taifa hilo wanalowea kwa muda mrefu bila kurudi katika mataifa yao.
Makundi ya viza
Tafsiri ya lugha ya kidiplomasia ya aina za viza za Marekani za B-1, B-2, F, M, na J zinaweza kuelezewa kama ifuatavyo:
Viza ya B-1 (Mgeni wa Biashara)
Viza hii hutolewa kwa raia wa kigeni wanaotaka kuingia Marekani kwa muda kwa ajili ya shughuli halali za kibiashara au kitaaluma, bila kujihusisha na ajira yenye malipo.
Viza ya B-2 (Mgeni wa kutembea)
Viza hii hutolewa kwa watu wanaosafiri kwenda Marekani kwa madhumuni ya utalii, mapumziko, matibabu au kutembelea familia na marafiki, kwa kipindi cha muda.
Viza ya F (Mwanafunzi wa masomo ya kitaaluma)
Viza ya F imetengwa kwa wanafunzi wa kimataifa waliokubaliwa katika taasisi za elimu zilizoidhinishwa nchini Marekani na wanaokusudia kusoma masomo ya kitaaluma kwa muda wote.
Viza ya M (Mwanafunzi wa mafunzo ya ufundi au yasiyo ya kitaaluma)
Viza hii inahusu watu waliojiandikisha katika programu zinazotambulika za mafunzo ya ufundi au kiufundi nchini Marekani, zisizo za masomo ya kitaaluma au lugha.
Viza ya J (Mgeni wa kubadilishana uzoefu)
Viza ya J hutolewa kwa washiriki wa programu zilizoidhinishwa za kubadilishana kitamaduni na kielimu, ikiwamo wasomi, watafiti, wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo (interns), na wataalamu wengine, kwa lengo la kuimarisha uelewano wa pamoja