Naveed Akram, mwenye umri wa miaka 24 ameshtakiwa baada ya kuamka kutoka kwenye hali ya kutokuwa na fahamu katika hospitali moja ya Sydney, Australia alikopelekwa baada ya polisi kumpiga risasi pamoja na baba yake ili kuwadhibiti wasiendelee kufanya mauaji.

Baba yake Sajid Akram, mwenye umri wa miaka 50 alifariki katika eneo la tukio.

Haya yanajiri wakati ambapo mamia ya waombolezaji wakianza shughuli za maziko ya wapendwa wao walioangamia wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi katika sikukuu ya Wayahudi ya Hannukah katika ufukwe huo.

Watu 15 waliuwawa huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa vibaya na bado wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Inadaiwa kuwa watu wote waliouwawa walikuwa Wayahudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *