#PichaYangSeries RADHIA @nana_dollz

Binti aliyekua pasina malezi ya baba na mama..anachukuliwa kituo cha kulelea watoto na kupelekwa nje ya nchi ambako anakulia na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo ujasusi unaombatana na mafunzo ya mapigano yaani ngumi, mkono, vitasa vyovyote utakavyoita.

Bila kujua anarudi kuanza maisha mapya Tanzania na jambo la kwanza ni kufanya kazi ya uokozi wa mtu muhimu. Kazi ambayo anapewa na shirika linalomuajiri la AIA.

Baada ya uokozi huo RADHIA, anagundua aliyemuokoa ni baba yake mzazi (Mzee Maega) na aliyekuwa amemteka ni baba yake mdogo (Mzee Maige) wakigombania hazina ambayo kila mmoja anasema ni yake.

RADHIA haelewi kwanini ana ‘tattoo’ mgongoni mwake na kila akijaribu kumuuliza baba yake ambaye kwa sasa anaishi naye pamoja na mdogo wake CHAICHAKA, mzee anamwambia usijali utajua tu.

Siku zinasonga kuna kijana anakuja kwao kama msaidizi wa kazi za nje, anaanza kuonesha kuvutiwa naye, kijana huyo ni Mussa ila amejitambulisha kama Sheiza akiwa na lengo la upelelezi kwenye kasri la Mzee Maega.

Mambo yatakuwaje kati yao? Kumbuka wote ni majasusi hatari…

Tukutane kila Jumatatu hadi Alhamisi kwenye #PichaYangu ya #SinemaZetu saa 1:30 usiku.

#HakikaNiZaKwetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *