Duru za habari ndani ya Sudan jana ziliarifu kuwa takriban raia 2,000 wameyaacha makazi yao katika mji wa Heglig wa magharibi mwa Sudan huko Kordofan Magharibi baada ya safari ngumu ya siku tisa ya kuhama makazi yao kufuatia kutekwa mji huo nawanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).

Qamarudin Mohamed gava wa jimbo la White Nile ameeleza kuwa wakimbizi 1,850 wamewasili katika mji wa Kosti wakitokea Kordofan magharibi. 

Kamishna wa Misaada ya Kibinadamu katika jimbo la White Nile Lamyaa Ahmed Abdullah amesema kuwa taasisi za taifa,  makundi ya kiraiana wafadhili wa ndani wameanza kutoa msaada wa chakula, malazi, na huduma za matibabu kwa raia waliokimbia makazi yao.

Wimbi jipya la raia kuhama makazi yao linashuhudiwa baada ya kikosi cha RSF kuudhibiti wa mji wa Heglig na kisima chake cha mafuta wiki jana. 

Majimbo matatu ya Kordofan Kaskazini, Magharibi na Kusini  yameshuhudia mapigano makali ya wiki kadhaa kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia kuhepa mapigano.

Wanamgambo wa RSF wanadhibiti majimbo yote matano ya eneo la Darfur magharibi, isipokuwa baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Darfur Kaskazini ambayo yamesalia chini ya udhibiti wa jeshi kati ya majimbo 18 ya Sudan.

Mkabala wake, jeshi la Sudan linashikilia maeneo mengi  katika majimbo 13 yaliyosalia kusini, kaskazini, mashariki na katikati, pamoja na mji mkuu, Khartoum.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *