Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham ziko mbioni kumsaka winga wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Bournemouth Antoine Semenyo, 25, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 65 ambacho kinaweza kutumika wakati wa usajili wa Januari. (Talksport)

Manchester United inaweza kumuuza mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, ambaye analengwa na Roma, ili kufadhili mpango wa kumnunua Semenyo. (Mail – usajili unahitajika)

Winga wa Chelsea Tyrique George anataka kuondoka The Blues mwezi Januari na timu kadhaa za Ligi ya Premia, pamoja na RB Leipzig na Roma, zinatazamia kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa Under-21. (CaughtOffside)

Everton wanamtaka kiungo wa Middlesbrough Hayden Hackney lakini huenda wakakabiliwa na changamoto kumsajili mchezaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari. (Team talk)

Aston Villa inajiandaa kufanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 28, kuhusu kandarasi mpya, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika 2028. (Football Insider)

West Ham inataka kumuuza mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Fullkrug huku AC Milan ikipigiwa upatu kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo wa miaka 32 mwezi Januari . (Guardian)

Youri Tielemans

Chanzo cha picha, Getty Images

AC Milan inaweza kumudu mkataba wa muda pekee kumsajili Fullkrug kutokana na mshahara wa Fullkrug – unaofikiriwa kuwa takriban pauni 100,000 kwa wiki – lakini klabu hiyo ya Italia ina nia ya kufanya uhamisho wake kuwa wa kudumu. (Givemesport)

Juventus inavutiwa na kiungo wa kati wa Marseille Pierre-Emile Hojbjerg lakini klabu hiyo ya Ufaransa inataka kumshikilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 30. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Arsenal inamtaka na beki wa AC Milan wa Italia Davide Bartesaghi, ambaye kandarasi yake ya sasa inaendelea hadi 2030. (Calciomercato – kwa Kiitaliano).

Manchester United imefufua upya mawasiliano na wawakilishi wa kiungo wa Trabzonspor Christ Inao Oulai. Manchester City pia inavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19. (Team talk)

Aston Villa haina nia ya kumuuza kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Lamare Bogarde, 21, licha ya Brighton kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Football Insider)

Inter Miami iko katika hatua za mwisho kumpa mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez mkataba mpya ambao utamuwezesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 kusalia klabu hiyo kwa msimu wa 2026. (Athletic – Usajili unahitajika)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *